Nitarejea

Hawa Ntarejea, Diamond Platnumz

[Intro: Diamond Platnumz]
Ah ah ah...

[Verse 1: Diamond Platnumz]
Vipi mizigo umeshaweka tayari
Mmmh, ah ah
Sijechelewa nkaachwa na gari
Mmmh, ah ah
Basi jikaze usilie mpenzi
Ah ah ah
Mi nitarudi niombee kwa mwenyezi
Ah ah ah
Zile taabu na njaa
Msimu mzima mavuno hakuna
Huwa nakosa raha
Pale mkikosa cha kutafuna
Roho yangu inauma
Sema ntafanya nini
Na pesa sina
Nakuonea na huruma
Bora niende mjini
Kusaka tumaa

[Chorus: Diamond Platnumz]
Kama watoto wakinililia (kama)
Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama)
Wadanganye na vibagia (wadanganye)
Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama)
Kama watoto wakinililia (kama)
Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama)
Nawe usichoke kuvumilia (usichoke)
Na kila siku kuniombea (nirude salama)

[Verse 2: Hawa & Diamond Platnumz]
Wanajua kwamba nafsi na roho
Vitakuwa na wasiwasi...
Ukumbuke na moyo
Utajawa na simanzi...
Ntakapokuwa nakwenda shambani
Afu niko peke yangu honey
Ntapokuja kuwa na majirani nitaumia
Ah ah ah...
Pale napotoka kisimani (ah ah)
Ama nipo na kuni kichwani (ah ah)
Sina wakunitua nyumbani nitalia
Maneno yako yananfanya nakosa raha
Na mawazo
Hata mwenzako sijawahi kufika Dar
Huu ndio mwanzo
Vile nakwenda na sijui pa kukaa
Wala mavasi, oh oh
We niombee niepushwe na balaa
Na maradhi, oh oh
Eh eh

[Chorus: Diamond Platnumz]
Kama watoto wakinililia (kama)
Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama)
Wadanganye na vibagia (wadanganye)
Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama)
Kama watoto wakinililia (kama)
Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama)
Nawe usichoke kuvumilia (usichoke)
Na kila siku kuniombea (nirude salama)

[Bridge: Hawa & Diamond Platnumz]
Unapokwenda kama ukifika salama
Utukumbuke na sisi
Usisahau kama mkeo na wana
Umetuacha na dhiki
Vile usijali ila naomba chunga sana
Ogopa na marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama
Waambie sidanganyiki
Unapokwenda kama ukifika salama
Utukumbuke na sisi
Usisahau kama mkeo na wana
Umetuacha na dhiki
Vile usijali ila naomba chunga sana
Ogopa na marafiki
Wakikulaghai hata kwa mbegu za mtama
Waambie sidanganyiki
Eh eh

[Interlude: Diamond Platnumz]
Nitrarejea mama
Niombee nirude salama
Oh, watoto wadanganye
Hii...
Ooh ooh ooh, oh oh
Tusale
Usijali
Hmm, kama...

[Chorus: Diamond Platnumz]
Kama watoto wakinililia (kama)
Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama)
Wadanganye na vibagia (wadanganye)
Waambie pipi ntawaletea (ntawaletea mama)
Kama watoto wakinililia (kama)
Waambie kesho nitarejea (nitarejea mama)
Nawe usichoke kuvumilia (usichoke)
Na kila siku kuniombea (nirude salama)

Wissenswertes über das Lied Nitarejea von Diamond Platnumz

Wann wurde das Lied “Nitarejea” von Diamond Platnumz veröffentlicht?
Das Lied Nitarejea wurde im Jahr 2010, auf dem Album “Kamwambie” veröffentlicht.
Wer hat das Lied “Nitarejea” von Diamond Platnumz komponiert?
Das Lied “Nitarejea” von Diamond Platnumz wurde von Hawa Ntarejea, Diamond Platnumz komponiert.

Beliebteste Lieder von Diamond Platnumz

Andere Künstler von Electro pop