Mchepuko

Mtoto wa kike punguza sifa
Unavyojituma hadi unatoa mishipa
Wana ni wangu ila unavyojipandisha
Viuno ni vingi chunga isije katika
Hujui kama tuko kwenye ndoa
Au umepanga kunikomoa
Unavyomganda hadi unaboa
Na una waganga kila mkoa

Anakusifia kiuno
Na unavyotoa miguno
Wake mfano sugunyo
Hadi unasahau kurudi nyumbani

Una mafuta na asali
Ukipandaga hushuki una hatari
Uvunguni juu ya dari
Leo nimekufuma hii show utakubali

Mchepuko mchepuko we
Mchepuko niachie baby wangu
Mchepuko mchepuko we
Mchepuko hebu muache mume wangu
Sa nisikilize bibi koma
Simu za usiku zimezidu koma
Unajifanya Beyonce wa kijiji koma
Eti una viuno vya Shakira koma
Hujui unanitia hasira eeeh
Ntakukata shingo

Baby hasira hasara
Usikunje ngumi acha kuchimba mikwara
Huyu anaitwa Sara
Mtoto wa dada kutoka Mbezi Kimara
Basi punguza papara
Viwembe vya nini umnyoe mwenzio kipara
Wanawake wawili msala
Nimejua ninu kilimshinda Manara

Iiih si wanaume eeeh
Si wanaume eeeh
Sio wasaliti mnatusingizia
Si wanaume eeeh
Si wanaume eeeh
Ni vishawishi ndo vinatuzingua

Baby acha basi minuno
Unataka vunja mtu kiuno
Kuchwa visa sio mfumo
Usije kuua uende gerezani

Umechafukwa una makali
Mama usinimwagie tindikali
Hiyo bunduki ni hatari
Ona mtoto wa kike huogopi serikali

Mchepuko mchepuko we
Mchepuko niachie baby wangu
Mchepuko mchepuko we
Mchepuko hebu muache mume wangu
Sa nisikilize bibi koma
Simu za usiku zimezidu koma
Unajifanya Beyonce wa kijiji koma
Eti una viuno vya Shakira koma
Hujui unanitia hasira eeeh
Ntakukata shingo

Beliebteste Lieder von Rayvanny

Andere Künstler von Afrobeats